Masista wa UrsulaESPANSIONE-descrizione in lingua italianawa Tanzania

 

Jubilei ya miaka 150 tangu alipozaliwa


Mtakatifu Ursula 1865-1939

Katika mwaka huu wa jubilei, tunataka, awali ya yote, kumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi ya Mtakatifu Ursula, aliyotoa sio tu kwa Shirika letu, bali hata kwa Kanisa zima na dunia.
 

Kwa mpango na kwa Maongozi ya Mungu, maadhimisho ya miaka 150 ya kuzaliwa kwa Mtakatifu Ursula, yako katika Mwaka wa Watawa. Wakati wa maadhimisho mengi yanayopangwa kufanyika  sehemu mbalimbali za dunia ambapo sisi tunaishi na kufanya kazi, tusisahau kumshukuru Mungu kwa ajili ya wito wa kila mmoja wetu na kwa ajili ya wawekwa wakfu  wote, ambao bila kukoma, katika  karne nyingi, wanashuhudia upendo wa kipekee kwa ajili ya Kristo na Kanisa, na wanatolea  maisha yao ili kuwapelekea msaada wote wanaohitaji. Kati yao, hata katika nyakati zetu, kuna mashahidi wengi, wanaoshuhudia upendo hadi kumwaga damu kwa ajili ya Kristo na Neno lake.
…Tukiuangalia mfano wa Mt. Ursula, ambaye maisha yake yaligeuzwa na kutafakari kwa mfululizo fumbo la  Moyo Mtakatifu wa Yesu Mteswa, tunataka hata sisi  kumwiga, tukichukua nafasi ya chochote kinachotokea katika maisha ya kila siku, ili tuweze kukigeuza kiwe  zawadi ya upendo kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya kila mtu tunayekutana naye.
 

Tujifunze  kutoka kwake  jinsi ya kuweza  kusikiliza maneno  ya Yesu “NAONA KIU”  ili sala yetu, mateso yetu, utulivu wa moyo na uaminifu wetu  katika kutekeleza majukumu tuliyokabidhiwa, ziweze kukidhi yale matarajio ambayo  Mungu ameyaweka juu ya kila mmoja wetu na juu ya Shirika letu lote.
 

Tufungue  mioyo yetu na pia jumuiya zetu kwa mahitaji ya mazingira ambapo tunaishi na kufanya kazi. Tuwe na ujasiri, kama Mwanzilishi wetu Mtakatifu, wa kwenda katika pembe zote za dunia alipo binadamu, jambo ambalo Papa Francisco analisisitiza sana kwa Kanisa zima. Wote tunapaswa  kuwajibika kwa ajili ya kazi kubwa ya uinjilishaji wa Kanisa la nyakati zetu. Tusisubiri wakati mzuri zaidi, maandalizi ya kielimu au afya bora zaidi. Katiba yetu, katika n.  85 inasema kwamba: “…kila mmoja wetu, yoyote iwe  kazi anayofanya  katika  jumuiya,  anashirikishwa katika utume kwa njia ya maelekeo yake ya ndani. Kwa njia ya maelekeo hayo,  sala yake, matendo ama ugonjwa vinapata umaana wa kitume.”
 

Hata sisi tuwe na ile tamaa kubwa ambayo tangu mwanzo wa maisha ya kitawa, lilikuwa wazo ambalo limeongoza maisha ya Mt. Ursula: ningejua kupenda tu …na kuwapa wote Mungu!  Tamaa hii imetekelezwa kikamilifu katika maisha yake, na hayo yamehakikishwa na maneno ya watu wengi ambao walimfahamu na pia kwa sababu Mama Kanisa aliamua kumtangaza Mtakatifu
Mwaka huu, uwe nafasi sio tu ya kumshukuru Mungu kwa Sherehe na  maadhimisho  mbalimbali, lakini pia kufanya utafiti wa moyo binafsi na wa jumuiya. Tuwe na ujasiri wa kujiweka mbele ya Mungu na mbele ya jumuiya katika ukweli  ili shukrani yetu kwa ajili ya zawadi ya Mt.  Ursula, iwe yenye matunda mengi zaidi kwa ajili yetu, kwa ajili ya Shirika na  kwa ajili ya Kanisa zima.
Tufikiri pia juu ya  zawadi za kiroho ambazo tungependa kumzawadia Mwanzilishi wetu katika  siku yake ya kuzaliwa…

Nawasalimia kwa upendo

M.Franciszka Sagun