Wosia


MAAGIZO YA MAMA MZEE KWA WATOTO WAKE WAPENDWA

Watoto wangu wapendwa, ninyi mnaelewa jinsi ninavyowapenda na kadri ilivyo katika moyo wangu ya roho zenu.

            Ningependa kwa hiyo kuwaachieni baadhi ya mawazo ambayo yanatoka katika moyo uliojaa upendo sababu itawasaidia kushika kufuata ile njia ya Mungu mwenyewe, kupitia zile, hali, ambazo ametutayarishia sisi, kwa shirika letu.

            Sio labda kwa upendo wangu, ukosefu wa unyenyekevu, naandika huu wosia wangu kumuiga kweli Mama na Mwanzilishi wetu Mtakatifu Angela?

            Nimepatwa na huo woga, lakini upende nilio nao kwenu umeshinda. Linarudi kwa dhati wazo la kuwaachieni kama wosia mawaidha yangu, mawazo yangu, ambayo niko tayari kwa kazi hiyo katika Jina la Bwana.

            Wanangu wapenzi, haya maneno ya Mama yenu mzee ambae ninyi mnampenda kidogo yatakuwa kwenu kweli yana maana na labda yatasaidia baadhi yenu kwa kuelekea upande mwema. Hata katika moyo wa mmoja yatawasha cheche za upendo kwa Mungu, itakuwa kwangu furaha kubwa.

            Kwa kila namna naandika kwa nia zaidi, kwa upendo mkubwa zaidi kwa Mungu na kwenu, watoto wangu. Nategemea kwamba Bwana atapokea mapenzi yangu mema na atabariki kazi yangu.

            Bwana awe nanyi, wanangu wapenzi. Nakumbatia na navuta moyoni mwangu kila mmoja wenu, na kwa kila mmoja naomba msamaha kwa maudhi, ambayo labda kwa udafifu wa maumbile ya kibinadamu nimeyafanya na kwa mifano mibaya ambayo kwa wakati mwingine nimewapa, kwa jinsi yangu ya kutenda ambavyo sio daima imekuwa sawa na kile nilichosema na hicho ambacho nawaandikieni sasa.

            Nawaomba kwa unyenyekevu mnisamehe yote kwa jina kubwa la upendo wa ki mama ambao ninao, na unanisukuma, kama mimi mwenyewe sio mkamilifu, napenda kuwaona ninyi watakatifu na wakamilifu.

            Kwa utakatifu wenu na wema wenu mlipie kwa Mungu ukosefu wangu wa utakatifu na wema. Kwa namna hii wanangu wapenzi mtashiriki katika utukufu wa Mungu na mtafupisha muda wa toharani wa Mama yenu mzee ambae anatamani sana kuunganika mapema na Bwana.

            Nawaambieni kwa heri wanangu, nitawaombeeni daima, na katika Moyo wa Kristo nitakuwa karibu nikiunganika nanyi.

            Mama yenu mzee hataacha kusali kwa ajili yenu ili tukutane siku moja wote pamoja mbinguni, kwenye miguu ya Yesu na ya Maria.

            Nitasali kwa ajili ya Shirika letu ili muweze kuendeleza kazi kwa ajili moja tu "kwa utukufu wa Mungu" na kwa ajili ya mema ya roho.

            Hodari na waaminifu wanangu wapendwa. Kama mwili wangu utakuwa ndani ya kaburi, roho yangu itakuwa pamoja nanyi. Nawapenda na nawabariki.

            Endeleeni mbele kwa uhodari kwa njia ya wema. Mioyo yenu iwe juu! Kuweni na amani! 

            Moyo wa Kristu upo pamoja nanyi. Katika Moyo wake Mtukufu tumeunganika pamoja.