WOSIA
I. AGIZO LA KWANZA
UPENDO KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU
Jambo la kwanza na wosia wa shauku zaidi ambao nawaelekeza watoto wangu ni huu: Pendeni, pendeni daima zaidi kwa moyo wa moto, wa mapendo Moyo Mtukufu wa Yesu, kupitia Moyo Safi wa Maria.
Bwana ameniteua mimi, maskini kutoa maisha kwa tawi hili jipya ambalo limetokana na shina la wa Ursula wa Zamani. Ambalo ni changa zaidi na dhaifu zaidi, la pekee na mali ya Moyo mwema wa Yesu.
Kwa hiyo wajibu wetu mkubwa sana wanangu ni kuupenda huo Moyo Mtukufu kwa nguvu zetu zote.
Tuupendeni huo Moyo Mtukufu. Maisha yetu na yawe ni kuendelea kuupenda huo Moyo mwema sana wa Yesu.
Ili muweze kupenda, ombeni huu upendo. Mapendeleo ya maombi yenu yawe katika sala hii (rehema ya siku 300). "Moyo Mtukufu wa Yesu nifanye nikupende daima zaidi".
Ombeni kwa ajili yenu wenyewe, na kwa kila sista, huo moto wa upendo na juhudi kwa Moyo wa Yesu. Upendo wenu kwa Moyo wa Yesu utawale mawazo yenu yaelekee daima zaidi kwake.
Kitu mkipendacho katika mawazo yenu kiwe ni Moyo Mtakatifu wa Yesu. Upendo kwake Yeye uamshe ndani ya mioyo yenu imani ya mtu ambaye, kwa amani ya ndani, anangojea yote toka kwa Moyo Mtakatifu sana wa Yesu.
Litokee lile litokealo: Ninyi bakini katika ukweli wa heri ambao Moyo wa Yesu atawaongoza kwa njia njema hata kama imeoteshwa miiba.
Msipoteze kamwe utulivu wa moyo ambao umepumzika katika Moyo wa Kristo, wala imani ya kutikisika kwa maana yote yataendelea vizuri sababu Yeye anaongoza kila kitu kwa mapenzi yake.
Hii imani isiyotikisika, ya kitoto, utulivu na mojawapo ya majaribu makubwa ya upendo ambao tunaweza kutoa kwa Yesu.
Iweni na imani, wanangu, kuweni na imani, hata kama upeo wa maisha ungekuwa mweusi kama usiku.
Kuweni na imani! Yesu, Moyo wake, umeshinda ilimwengu na umaskini wake wote. "Msiogope, kundi dogo, kwa sababu Baba yenu amependa kuwapa Ufalme wake". (Lc.12,32)
Fanyeni sehemu ya ufalme wa Moyo wa Yesu, tafuteni kwa hiyo kitu kimoja tu; kuupanua huo utawala wa Moyo wa Yesu katika mioyo, na msihangaike na kitu kingine. Moyo wa Yesu chochote kile ambacho mnahitaji kwa ajili ya wokovu wenu. Hamhitaji kitu kingine chochote.
Tupatie ee Bwana, upendo, upendo ambao daima ni mkubwa zaidi na hiyo inatutosha.
Ningependa kuupenda kwa kweli ule Moyo Mtukufu kwa upendo ule ambao utakuwa kwake kitulizo, upendeni kupitia kwa Moyo Safi wa Maria Nyota yetu angavu ya baharini, ambayo kwa nuru ya mionzi yake inatuelekeza katika Jua, kwa Moyo mtamu wa Yesu.
Wakati mioyo yenu ikiwa baridi na gizani, angalieni Nyota yetu, jishikeni kwa Moyo safi wa Maria, mwombeni huyu Mama yetu kuangazia kwa mwanga wake, giza lenu, kwa kupasha joto mioyo yenu ili kuweza kuupenda zaidi na zaidi Moyo Mtukufu wa Yesu.
Na mwisho mshuhudieni kwa upendo wenu, kwa imani kabisa kwa kufuata wema wake. Mkimfuata mtaonyesha kuwa watumishi wake waaminifu, watumishi wampendao kuliko vitu vyote.
Katika maagizo yafuatayo, napenda watoto wangu, kuweka mbele ya macho yenu mema ya Moyo Mtukufu, nikiwaomba kwa muda huo: Wanangu fuateni, fuateni kwa uhodari wema wa Moyo wa Yesu, katika hayo ndipo kwenye upendo wenu, utukufu wenu wa milele.