WOSIA


XI. AGIZO LA KUMI NA MOJA

 

MAPENZI YA MUNGU

 

            Ulimwenguni hakuna cho chote kikubwa zaidi ya mapenzi ya Mungu.

            Kanuni takatifu ni nzuri sana kwetu sababu zinatuongoza, kila hatua, mapenzi ya Mungu kuyatimiza. Lakini yenyewe yanaweza kujionyesha hata kwa njia nyingine. Mungu anatuonyesha mapenzi yake kupitia njia mbali mbali za maisha, ambavyo haitegemeani na sisi, anatuonyesha mapenzi yake ili tuweze kuyafuata na kujinyenyekeza kwa yenyewe.

            Kama tunapenda kuunganika kabisa na mapenzi ya Mungu, tunapaswa kuyatimiza kwa uaminifu, kuyatimiza na kujinyenyekesha kwa yenyewe. Tunapaswa kuyakubali hata kabla hayajajitokeza, chochote kile Mungu anachopenda kutimiza kwetu sisi sababu kitu chochote afanyacho Mungu, ni daima kwa ajili ya mema yetu.

            Tukiishi kwa usalama katika mapenzi ya Mungu tukipigana dhidi ya faghaa, mahangaiko, woga kwa wakati mwingine, haswa kwa hatari inayotokea kwa ghafla au mateso, haya mapenzi ya Mungu yanayo uwezo zaidi.

            Kwa nini wafadhaika? Kwa nini unahangaika? Itakuwa kile Mungu apendacho, na itakuwa vyema.

Kama Mungu apendavyo!

Haya meneno yatamkeni kwa upendo, yenyewe ni faraja kwa roho iliyo na uchungu. Yarudieni wakati mkiwa na fadhaa, yarudieni wakati Mungu anapowapatieni msalaba.

 

            Kwa hiyo sio tu kukubali mapenzi ya Mungu bali jinyenyekesheni kwa yenyewe kimya kimya, bila kulalamika, kwa tabasamu la mdomo, na kwa "Deo gratias"- Tumshukuru Mungu- ndani ya moyo.

Kama Mungu apendavyo!

Huu msalaba ni mapenzi ya Mungu na mapenzi ya Mungu ni hazina yetu kubwa duniani, ni furaha ya moyoni inayompenda Mungu.

Kama Mungu apendavyo!

Pendeni mapenzi ya Mungu, kanyageni kwa uhodari lile ganda gumu na chungu Mungu amewapeni. Na mtajikuta mmeingia katika kiini cha mapenzi yake, mzigo wa wema na mtamu.

            Mwanangu unapenda kuunganika kabisa kwa undani na Mungu? Yatimize kwa uaminifu mapenzi yake, yakubali kwa upendo, nyenyekea kwa yenyewe kwa uhodari na furaha, na hivi utajiunga katika ncha ya utakatifu.

            Sala, kitubio, upendondizo zilizo 

katika mstari mkubwa wa maisha ya kitawa.

 

Kumbuka kwamba: 

Sala iliyo bora zaidi: ni kujiweka kwenye mapenzi ya Mungu.

Kitubio kilicho bora zaidi ni kujiweka kimya kimya katika mapenzi ya Mungu.

Upendo ulio mkubwa zaidi ni kutimiza kwa uaminifu mapenzi ya Mungu.

            Kama Mungu apendavyo! Kama Mungu apendavyo! Kua maneno haya mdomoni utaishi maisha ya utulivu hata kwenye dhoruba; furaha hata kwenye shida, upendo hata penye chuki, mtakatifu kwenye dhambi, mtukufu ungali bado duniani.

 

            Kama Mungu apendavyo!