WOSIA
XII. AGIZO LA KUMI NA MBILI
UTULIVU WA ROHO
Mmoja wa wakubwa wa waandishi wa maisha ya kiroho aliandika kwamba, kuwa daima na utulivu moyoni ni kitubio kikubwa zaidi. Na ni kweli, kwa sababu inahitaji nguvu nyngi za kujitoa kwa kujitawala mwenyewe, kwa kujihini, kwa kuwa daima mtulivu, kama nuru, mwenye furaha, mtulivu japo una shida, ujisikiapo mgonjwa, wasi wasi, ukiwa na taabu.
Kwa vingine huu utulivu wa rohoni, hii furaha ya ndani ni msaada mkubwa sana kwa kazi ya kiroho. Ni kwa roho kile ambacho ni kama jua kwa ardhi.
Kama kwa kitendo cha mionzi ya jua maua yanachanua na mutunda yanakomaa, hivi katika moyo uliotulia, wenye furaha, una kuza ua la kushangaza la utakatifu linaloongeza kuzaa matunda ya wema.
Jua katika mbingu, moyo wenye furaha duniani ni heri kiasi gani wanatoa kwa wanadamu, ni kitulizo kiasi gani kwa mioyo!
Labda kitendo kikubwa cha upendo kwa ndugu ni uvumilivu wa moyoni daima ambao unaeneza karibu nawe mwanga na joto.
Mtu mwagavu wa furaha, anapita Kimya kama mionzi ya jua- aona uchungu kwamba hafanyi lolote jema- sababu hajuni kwamba ameamsha kwa utulivu wake tabasamu nyingi za wasi katika- vinywa vya wengine, kwamba amemimina katika mioyo Mingi faraja na kitulizo, kuwa amewasha moto mioyo iliyokuwa baridi, asiyependelea, kuwa ameondoa mawingu giza, kwa wale wasio na tumaini hadi wame kata tamaa, kuwa anaotesha bila kufahamu furaha nyingi kando kando yake.
Yeye hafahamu, bali Mungu anafahamu. Ni Mungu anampatia ustahimilifu wa furaha ambayo ametoa kwa wengine. Inahitaji kwa kweli nguvu nyingi za kiroho kwa kuweza kushikilia huu ung'ao wa utulivu.
Sio rahisi kuwa mwenye furaha, wakati ambapo mahangaiko yanatuchokesha, wakati watu wakituchoka na kutusumbua, wakati ulegevuu wa kazi hautuachii nafasi ya kupumzika, wakati magonjwa yanatupunguzia nguvu na uchungu wa kimwili yanatuumiza wakati tunapojisikia kuanguka chini ya mzigo msalaba.
Hapana sio rahisi!
Ni kwa yule tu anayeunganisha mapenzi yake na ya Mungu, ni yule tu anayetafuta furaha katika mapenzi ya Bwana aliye juu mbinguni, kuhifadhi ndani yake huu utulivu mtakatifu, huu uwazi, furaha yenye mwangaza usio wa kawaida, usio wa kidunia.
Mtoto wangu kama umeingia shirikani kumtafuta Mungu unapaswa kutafuta furaha sababu unayo chem chem yenyewe ya furaha, unae Yesu Kwenye Tabernakolo, Yesu katika komunyo ya kila siku. Umezungukwa map enzi ya Mungu. Umekosa nini tena kwa kuwa na furaha?
Kama ungetambua na kuelewa hii furaha ya maisha ya kitawa, utakuwa, bila shaka lolote na furaha. Na furaha yako haitategemeana mambo ya nje, itamulika kwa nje na kutia joto moyoni mwako. Kama namna hiyo utakuwa "mwangavu".
Mpende Yesu, mpende juu msalabani, mpende kwenye Tabernakolo, mpende katika mapenzi ya Mungu, na utakuwa daima mwenye furaha; na hii furaha itakugeuza kuwa jua kwa ajili ya wengine, hata na Yesu ambae amezungukwa na Tabernakolo ya ubaridi na upweke. Sio labda huo ndio wa kushangaza.
Kumbuka kwamba mtu mwenye furaha, yeye mwenyewe ni mtume ambae, bila kufahamu anaji peleka kwa Mungu, sababu anaelezea kwa wanadamu bila maneno, bali kwa tabasamu angavu ambalo ni jema, jema sana kumtumikia Mungu ina maana kusema kwamba hauwezi kuitoa.
Watoto wangu, iweni wenye furaha, waangavu, watulivu na mtaufurahisha Moyo wa Kristo; Mtakuwa kitulizo kwa wakubwa wenu, na wenzenu, na kwa watu wote ambao mtakaa nao.
Kilicho cha maana zaidi yatimizeni kwa furaha mapenzi ya Mungu ambae, kama asemavyo Mtakatifu Paulo; Utakatifu wenu: "... haya ni mapenzi ya Mungu, kutakatifuzwa kwenu" (1 Ts.4,3).
Kwa hiyo daima watulivu, wenye furaha twendeni kwa imani kumwuelekea Mungu!