WOSIA


XIII. AGIZO LA KUMI NA TATU

 

EKARISTI TAKATIFU

 

            Wanangu wapendwa, Yesu kakika Tabernakolo ni jua kwa maisha yetu, utajiri wetu, furaha yetu na kila kitu kwetu duniani.

            Furaha ya mtawa ipo kwenye mapenzi ya Mungu na katika Ekaristi Takatifu.

 

            Kama ukitimiza kwa uaminifu mapenzi ya Mungu itakuwa vyema kukaa mbele ya Tabernakolo!

            Yesu akiona unatimiza mapenzi yake atakupenda, atakuja kwako atakaa katika moyo wako uliounganika kabisa na mapenzi Yake na unaweza kusema hivi: "Sio mimi ninaye ishi tena bali ni Kristo anaishi ndani yangu" (Gal. 2,20).

            Mpendeni Yesu katika Tabernakolo!

Pale ibaki daima mioyo yenu, hata kama kimwili mko kazini. Pale yupo Yesu, ambapo twapaswa kumpenda kwa u moto kwa moyo wote. Na kama hatumfahamu kumpenda, tutamani kumpenda daima zaidi.

            Komunyo takatifu iwe ni kiini, tulicho nacho kati yetu ambacho kinatufungulia kila siku kwa maisha yetu yote.

            Wakati wa maana zaidi katika siku ni ule wakati wa komunyo takatifu, wakati ambao Mungu wetu na Bwana anakuja upya kumiliki katika moyo wetu maskini.

            Unajifungua kabisa kwa Bwana Wetu mkubwa, huru kwa tamaa zote za duniani, kwa kuhukumu, kwa kutamani makuu, wasi wasi, mawazo ya kidunia.

            Yote ndani yenu ni kimya, aongee Bwana. Bwana alinde, Bwana atawale, Yeye tu aishi ndani yenu.

            Jishikeni kwa Yesu kama wakate Magdalena alipokuwa kwenye miguu yake. Sahauni yote katika ule wakati mpendelevu, na kuweko na Yesu na ombeni, ombeni kwa moyo wa bidii, kwa bidii hata kwa Kusisitiza: "Yesu nipatie upendo daima mkubwa zaidi".

            Yeye kwa kweli alisema: "Ombeni mtapewa" (Mt.7,7). Ombeni basi, mkiwa na uhakika kuwa Yesu atawasikiliza.

            Na wakati wa mchana, moyo wenu tangu asubuhi hadi jioni, uelekee tabernacolo. Jaribuni! Hii tabia inapaswa kushinda, na inawezekana kuipata na kujiunga nayo.

            Unaweza kuisalimu Sakramenti kwa kiroho, hata kama kwa mwili uko mbali, kwenye kazi.

            Wakati inapowezekana menda na amkia mara moja mara mbili au zaidi kutokana na jinsi uwezavyo na unayo ruhusa.

            Nenda kwa Yesu kama mtoto kwa mama, kama rafiki mwenye huzuni na mchovu kwa rafiki yake, ambapo ndipo kiini cha kupata kitulizo na msaeda.

            Nenda na mwambie Yesu wako chochote kile kilichoke moyoni. Wewe humwoni, bali Yeye yule pale katika tabernakolo. Hii unaweza kuamini hata zaidi ya kuweko wewe.

            Na wakati unapiga magoti mbele ya tabernakolo na huelewi ufikiri nini, au unapotewa na mawazo nyenyekea kabisa undani.

            Wewe uko pale kama kitambaa cha nguo ambayo haijaoshwa, na huwezi chochote, bali jitoe wazi kimya kimya, kwa unyenyekevu, umaskini wako kwenye kitendo cha mionzi ya upendo ambayo inatoka kwenye tabernakolo. Ni kama jua linavyofanya nguo kuwa nyeupe, hivi Yesu ataifanya mioyo yenu mieupe na mizuri.

 

            "Hata kama makosa yako yanakuogo pesha, hata kama unajisikia kuchoka kwa kumtumikia Yesu, Yeye jua lako atakuokoa, Yeye anafanya kazi kwa ajili yako, ili wewe ujiweke wazi kwake kwa kitendo cha mionzi yake".

            Baki katika ukimya, jitokeze kuelekea kwenye mionzi ya Jua lako Eukaristia. Hata kama unajiona kukufanya lolote, ngojea na uwe na imani. Yesu mwenyewe anafanya kazi katika roho yako. Usimkimbie.

            Na kwa wakati mwingine watoto wangu, uchungu mahangaiko, kufa moyo, vinapenya ndani ya moyo wako, jaribu kuviondoa, haswa basi nenda kwenye tabernakolo. Pale ndipo kwenye hazina yako.

            Zinawezaje kutudhuru hizi shida; na maudhi? Zenyewe haziwezi kukuletea Yesu, na mpaka uwe na Yesu unayo furaha katika Yeye, mwanga wa mbingu, na mbingu yenyewe. Wakati chochote kile cha duniani kitakuwa kidogo mbele ya huu ukweli.

            Na baadae wakati unapokuwa umepiga magoti mbele ya tabernakolo, fungua kabisa moyo wako, kwa huo upendo, baadaye kuwa na hakika kuwa Yesu atakubali wazo lake, hata kama wewe unajisikia umepoa na wa baridi. Yeye atakusaidia kufikia ule upendo ambao kwa moyo wako wote unautamani.

            Kubadili upendo wako usio kamili, na dhaifu, atakupa upendo ule mkubwa wa Moyo wake Mtukufu. Na wewe, mdogo, maskini, usiye kamili, "mdudu mdogo" utakuwa kitu cha upendo kwa Yesu wako, Mwokozi wako, Mungu wako, na unaweza kusema kwa hakika: "Yesu ananipenda".

            Ni mwema kiasi gani Yesu wetu!

Mpendeni kwa Sakramenti ya upendo! Yeye ni hazina yenu. Ishini kwa ajili yake. Kwa Yeye jishikeni wakati wa giza. Yesu awe kisima chenu cha furaha yenu duniani, wakati wote wa maisha yenu ya kitawa, na siku moja juu katika umilele.