WOSIA


XIV. AGIZO LA KUMI NA NNE

 

MKAZO WA FIKIRA NA UKIMYA

 

            Kama mnapenda wanangu kuwa karibu na Mungu, karibieni kwa Yesu wenu; mngeweza kujizoeza kwa mkazo wa fikira, kuwa waaminifu katika ukimya, wakati wa masikitiko katika kazi yenu.

Ukimya ni amani ya moyoni.

Shikeni ukimya wakati mnapo pokea kazi zenu, zungumzeni kile cha maana, lakini msizungumze kile kisicho cha maana. Heshimuni ile kimya kuu kama matayarisho ya komunyo takatifu. Ukimya uweke karibu kabisa na uheshimiwe utawani. Na inapokuwa ni lazima zungumzeni, na zungumzeni kwa sauti ya chini, ili msisumbue kimya cha wengine, ili wasijetoa mawazo yao kwa Mungu.

            Linapotua Jua siku yote, mwisho wa kazi zenu, wakati kengele inapoita kukaa kimya, maisha yetu tunayoishi, yanaacha kutosumbuliwa tunaanza maisha yetu na Mungu.

            Inua kadiri uwezavyo moyo wako kuelekea mbinguni Ingia katika ule ulimwengu mtukufu. Pale wanakungoja Yesu na Mama yako Mtakatifu, malaika mlinzi, na roho nyingi zinazokupenda. Zungumza na wakaaji wa Mkoa wa mbinguni. Omba, shukuru, tolea masumbufu yako, woga, matumaini, kwa Moyo mpenzi wa Yesu, kwa Moyo wa Maria.

 

            Na furahi vuta kwa mapafu yaliyojaa ile hewa ya u milele inayokunguka.

            Ni vyema kujitoa, hata kwa muda mfupi, kutoka duniani. Ndio ni vyema.

            Na wakati wa mchana wakati kazi zimetusonga sana, wakati mwingine unapaswa kuzungumza zaidi ya ulivyopenda, na ni shida kuunganika na Mungu, sababu inakupasa kufikiri ile kazi ambayo umepewa, kwa hiyo jaribu kila wakati, kuuelekeza moyo wako kwa Bwana, kwa kumwambia kuwa unampenda, kwa kufanya upya nia nzuri kwamba kila unachokifanya unafanya kwa kumpendeza Yeye tu. Kwamba maisha yako yote, kila kazi yako ni kwa Yeye tu, kwa Yeye peke yake.

            Huku kuinua moyo kumwelekea Mungu, hata kwa wakati mwingine,ina badili kazi kuwa sala, maisha yako ya duniani kwa maisha yasiyo ya dunia, ya utukufu.

            Usifikiri kufikia huo mkazo wa fikira na kuunganika na Mungu ni kwa muda mfupi tu. Hapana, ni kazi ya miaka mingi.

            Asubuhi azimia kwamba, wakati wa mchana, wakati mwingine, kwa mfano kutoka katika sehemu moja kwenda nyingine utainua moyo wako kwa Mungu.

            Wakati wa kuhoji dhamiri yako jiulize kama umetimiza hiyo ahadi kuifanya upya.

 

            Omba neema ya kuunganika na Mungu. Fanya kazi bila kukata tamaa, hata kama huoni matokeo.

            Pole pole bila ya wewe kutambua, moyo wako utaunganika daima zaidi na Mungu, na Kristo atakuwa daima zaidi kiini cha maisha yako.

            Jaribu kuunganika na huo mkazo mtakatifu wa fikira, ukikwepa kupayuka kusiko na maana, uchunguzi usio na maana.

            Kwa nini ufahamu yote? kadiri unavyofahamu kidogo yale yatokeayo karibu nawe, ndivyo zaidi itakuwa rahisi kwako kuhifadhi mawazo pamoja.

            Na usijiingize katika mambo ya wengine hivyo utaepuka na na wasi wasi mkubwa, na unaweza kufanya kazi na kusali kwa utulivu.

            "Ni voir ni etre vue, ignorer et etre ignorée". Hata kuona, hata kuonekana, msitafe kufahamika, kuweni msiojulikana. Ni furaha kwa roho inayoishi maisha haya.

            Sahau ulimwengu, jisahau haswa wewe mwenyewe. Ishi kimya kimya kwa ajili ya Yesu tu, katika yeye na pamoja na Yeye.

            Utafikia hiyo mbingu kama hapa duniani utajizoeza kwa uvumilivu na saburi, katika ukimya na katika fikara.