WOSIA
XV. AGIZO LA KUMI NA TANO
UKWELI KWA WAKUBWA
Kuweni wakweli wanangu, jinsi mtakavyokuwa wakweli mbele ya wakubwa wenu, ndivyo zaidi mtakavyokuwa kuwa wema.
Kanisa linawakataza wakubwa na hiyo ni haki, kuingia kwa nguvu katika siri ya mioyo ya masista waliokabidhiwa. Wala kwa maswali, wala kwa kuogofya, wala mvuto ambao wao watalazimika kufungua ufahamu wao wa nafsi. Lakini kila sista anayo haki ya kujiaminisha kwa sista mkubwa wake, na kumfahamisha kile kilicho chema na kibaya, kilichoko ndani yake, kwa sababu ni kwa njia hii sista mkubwa anaweza kumsaidia, na kumwongoza.
Na huu uongozi wa mkubwa ni kama egemeo kwa roho, ni kama kamti kadhaifu ambako, kila ukija upepo kanakunjika.
Ukweli sio wema kwa vijana tu, kwa wale wanao anza maisha ya kitawa, bali hata kwa wale walio wazee.
Katika maisha ya kiroho, tunapaswa kuwa kama watoto, na watoto wanahitaji mkono wa kimama.
Usiseme: "Ninae muungamishi kwa hiyo ananitosha". U kweli muungamishi mwema ni hazina kwa roho, walakini nakueleza kitu kimoja. Muungamishaji anakufahamu tu wakati wa kuungana. Lakini una hakika kuwa unajieleza kwa u kweli? Si kwa sababu unapenda kumdanganya, hapana; bali kwa upendo wako mwenyewe, kujipenda kwako kunakufanya kipofu. Wewe mwenyewe hujifahamu vizuri, bali mkubwa wako anakufahamu zaidi sababu anaona vile vitendo vya udhaifu ambavyo wewe huvioni.
Angeweza kwa wakati mwingine kukuepusha na mabaya, lakini hawezi sababu wewe unakaa mbali nae, huna imani nae, hupendi kana kwamba aingilie maisha yako ya ndani.
Dada zanguni, niaminini, anafikiri mara nyingine kwamba, yule anayeungama ni mtakatifu na ni Sadaka ya upendo, ambavyo mkubwa wako, lazima kwa bahati mbaya afikiri tofauti. Muungamishaji anasikia maneno tu, bali mkubwa wako anaona matendo.
U kweli hauna maana kwamba unapaswa kuongea kila dakika na Mkubwa wako, kumweleza maisha ya roho yako, kujipendelea kwa nafsi yako mwenyewe; Hapana!
Mimi namwita mkweli yule ambae hafanyi, hasemi chochote ambacho hakipaswi kueleweka kwa mkubwa wake. Ambae anaishi daima kana kwamba mkubwa wake anafahamu kila kitu anachofanya, anachoongea, hadi anachofikiri.
Na kwamba hamwahidi yeyote kutosema chochote kwa mkubwa. Kamwe!
Inawezekana kuwa mkweli sana mbele ya wakubwa, yule ambae mara chache anaongea kuhusu maisha yake ya kiroho. Na anaweza kukosa kuwa mkweli yule ambae anang'ang'ania, anamsumbua mkubwa kwa mazungumzo, sababu anaongea tu kile kimpendezacho, na anaficha kile ambacho hapendi kusema.
Nakushauri mtoto wangu, mfahamishe mkubwa wako kitu ambacho unafanya haswa; sio kwa sababu lazima akushauri yeye, hayo ni juu yako, bali wewe mweleze ili afahamu ni juu ya nini haswa unafanya kazi, na wakati mwingine yeye aweza kukusaidia.
Mjulishe mara kwa mara angalau kila baada ya miezi mitatu, haswa mtihani wako wa maisha, na utakuwa na msaada mkubwa kwa kuendelea katika kazi hiyo.
Omba wakati mwingine akuambie yale yote anayoyaona kwako yasiyo kamili, Pugufu, na akushauri jinsi ya mwenendo mwema ili kurekebisha kile ambacho hakiendi sawa sawa.
Acha uongozwe na mkubwa. Yeye ni egemeo ambalo Mungu mwenyewe ametoa kwa roho yako.
Usiangalie kuwa yeye ni mzee au kijana, wa kupendeka au hapana, bali kumbuka daima kuwa ni kwa shela moja tu ambayo kwayo, Bwana anakuelekeza na kukuongoza.
Kwa hiyo nenda kwake kwa imani ya kitoto. Kuwa mkweli. Hii ni njia ya uhakika zaidi. Kuwa kama alivyosema Mt. Yohani Berchmans (Weupe kama maji kwa wakubwa), na mtapata amani na furaha katika huku kuwa wakweli, kwa kuwa wenyewe unatusaidia kufikia kwenye ushindi.
Ukweli ni unyenyekevu, na unyenyekevu ni kisima cha neema, cha amani, cha utakatifu.
Kuanzia dakika ya kwanza ya kuingia Shirikani hadi mwisho, hata kama mngeishi miaka mia, kuweni wakweli, ule ukweli wa mtoto kwa wakubwa wake. Majivuno yasiwaache kamwe kukwepa hii njia ya uhakika.