WOSIA


XVI. AGIZO LA KUMI NA SITA

 

BIDII KWA AJILI YA UKOMBOZI WA MIOYO

 

            Ursulina mmoja wa Yesu Mteswa angepaswa kusikia maombi ya uchungu yatokayo katika kinywa cha Bwana ambae anateseka juu ya msalaba: "Sitio".

            Ni mlio wa uchungu utokao katika moyo uliojaa tele mateso kwa kikundi kidogo cha watu wanaofahamu kutumia nafasi kwa kupata neema ambazo Yeye, Yesu wetu, kwa mateso yake na kifo, amestahilia kwa ajili yetu na kwa kizazi chote cha ubinadamu.

            Yesu ana kiu, na hicho kiu ni kingi hivyo kwamba Yeye, hakulalamika kamwe, kana kwamba hangeweza kuzuia ule huzuni.

            Wanatamani watu wenye uwezo wa kumpenda kuhusu kuweka, katika kubadili upendo wao, kwa hazina za neema zake, kutoa katika furaha, ya umilele, mbinguni, ambapo anapenda kutayarisha nafasi kwa ajili yao.

            Watoto wangu, uwake katika mioyo yenu, mfulilizo wa moto kwa upendo wa nyoyo. Ziokoeni, zipelekeni kwa Yesu, wafahamisheni, wao ukubwa wa wema wa Moyo wake, haya wazo ambalo tunapaswa kujifunga nalo.

            Padre mmoja mtakatifu anaweza kufanya mengi sana kwa ajili ya kuziokoa roho; Salini basi kwa ajili ya mapadre ili Bwana atume wafanya kazi katika shamba lake.

            Msijiwekee kadiri katika huo ukamilifu wa kujitoa sadaka: Ule wa hiari ya nafasi ya kutamani makuu, heshima, uvivu. Kuweni wenye moyo wa ukarimu wa kujitolea sadaka kwa hawa mapadre wetu wadogo, "in spe".

            Ni neema ngapi anaweza kuomba kwa ajili ya mapadre Sista ambae kwa ukimya, hafahamiki na ulimwengu, anajitolea kwa kazi rahisi na zisizo tambulikana, anafanya kazi, anajitoa sadaka, anaweza kuvumilia kimya misalaba midogo ya maisha, na kwa kazi hiyo, uchovu, kujitolea sadaka kwa Bwana neema kwa ajili ya mapadre.

 

            Siku moja hukumu ya mwisho yeye ataona matunda ya ukimya wake, kutofahamiwa na ulimwengu kwa ajili ya ukombozi wa mioyo, kwa ajili ya ile sadaka ya "u mimi" kwa kupata neema na utakatifu kwa ajili ya mapadre.

            Wanangu, ni wazo gani la kushangaza! Na kama tunayo mbele yetu wazo kubwa, ni rahisi zaidi kazi na tuko tayari, zaidi kufanya kile ambacho maumbile yanapendelea.

            Wakati kwa mara kwanza nilipoenda kwa Baba Mtakatifu Pio XI, ambae alikuwa (nunzio apostolico) mjumbe wa Baba Mtakatifu wa Varsavia, yeye alinifanya nitafiti kwamba Bwana hakuomba kitu kingine cho chote kwa kusititiza sana kusali, kama kupata mapadre wema.

            Na wakati, kwa mara ya kwanza nilipopiga magoti kwenye kaburi la Mt. Pio X, Baba wa Shirika letu, Mfaranza mmoja nisiye mfahamu alinipa ile sala ya kuwaombea mapadre ambayo tunaisema kila siku.

            Sio labda hizi ishara wazi za mapenzi ya Mungu? Hajionyeshi kwetu Yesu kupitia kwa wasaidizi wake duniani mapenzi yake kusudi tusali kwa mamna ya pekee kwa kupata mapadre wema?

            Kwa uhodari basi, wanangu wapenzi, kwa vitendo, kwa uhodari!

            Wapaswa kuwa ile sadaka ambayo kimya kimya na kwa mfulilizo unatumika katika kazi, katika sala, katika kuteseka, kwa ajili ya kupata neema kwa ajili ya mapadre.

 

            Kila msalaba utakuwa mwepesi, kila maumivu yatakuwa mepesi, kila sadaka nzuri zaidi itapewa moyo na ombi hili: "Yesu pokea toleo hili ambalo linakulilia mbinguni Bwana tupatie mapadre wema na watakatifu".

            Waheshimuni mapadre, msiongee kamwe vibaya juu yao, hata kama wasipotenda vizuri, labda kama sababu ya kweli ambayo inakubidi kufanya hivyo.

 

            Msizungumze kati yenu, hata mapadre, hata waungamishaji, bali watoleeni kwa Bwana daima kwa heshima kubwa. Kwa vikwazo ambavyo kwa bahati mbaya, vinaweza kwa wakati mwingine kutokea kwa mapadre, ombeni msamaha kwa Mungu kwa nguvu zenu zote na jaribuni sana uchungu toka kwa majeruhi ambayo yanatokana na kutoneshwa na wale ambao wamechaguliwa kwa heshima kwa zawadi ya kipadre.

 

            Dada zangu, watoto wangu, msifikiri sana juu ya mateso yenu, ambayo wakati mwingine ni ya kubuni, kwa misalaba yenu kwa kawaida midogo ambayo upendo wa kibinafasi unashusha, sana hufunika kuuona Moyo wa Yesu Mteswa, ulioingia katika uchungu kwa kutoamini kwa watumishi wake.

            Utukufu wa matendo matukufu ni kushirikiana kwa kuziokoa roho. Kwa mimi inaonekana kwa hivyo kwamba ni utukufu zaidi ule wa ushirikiano, na kwa utakatifu wa mapadre, na kwa uongezekaji wa wito wa kipadri.

            Katika kazi ya maana hii wekeni kwa hiyo kwa upendo na sadaka! Katika kazi hiyo msichoke au kufa moyo, hata kama labda kamwe hamwoni hapa duniani matunda ya uchovu wenu.

            Ni afadhali zaidi! Yesu mwenyewe anakusanya matunda ya sadaka zenu.

            Wewe maskini dadangu, uliyefikiri kuwa usiofaa mtumishi wa Bwana, utaona mbinguni matunda ya kazi yako, ambayo Yesu atakulipia kwa upendo wake, na atakufurahisha kwa kukuonyesha roho ambazo umezipata kwa kazi yako, sadaka na kujitolea, neema na mwanga, kwa kutimiliza zaidi kwa uaminifu wajibu mtakatifu wa kipadre.