WOSIA
XVII. AGIZO LA KUMI NA SABA
UPENDO NA HESHIMA KWA MASHIRIKA
YOTE YA KITAWA
Inakanywa mara kwa mara kwa mashirika ya kitawa ambayo hayapatani kati yao. Hiyo inawakwaza walei na sifa mbaya kwa shirika.
Sio kazi yangu kutafuta sababu hizi za kutoelewana. Mara kwa mara inatokea kwa pande zote mbili, ingawaje kwa hiari inakuwa ni bidii ya zaidi yaogopwa, kwamba kivuli kingine kisije kuona uanzilishaji wa kazi zao.
Na wanasahau kwamba kazi kwa ajili ya Mungu ni nyingi ukilinganisha na kazi za Mungu zisizo na mwisho, ambayo namba ya mashirika ya kitawa mara mia zaidi ya sasa wanaweza kufanya kazi kwa utulivu bila kuingiliana wenyewe.
Watoto wangu, ningependelea muwe na moyo ulio wazi kwa kila shirika la kitawa. Kwa sababu kila mmoja wao ameundwa na watu waliojitakatifuza kwa Mungu ambao wanatumika katika sala, kwa sadaka, katika kazi kwa ajili Yake.
Utaachaje kuwapenda hawa watu, utaachaje kuwaheshimu!
Kiwe mbali nanyi kila kivuli cha wivu kwa maendeleo yao. Maendeleo yao ni maendeleo kwa ajili ya Mungu.
Sio hicho tunacho kitamani hata sisi?
Kwa kweli tunajitakia heri kwa maendeleo ya kazi yetu, sio kwa sababu ni yetu, bali kwa sababu tunafanya kazi kwa ajili ya Yesu. Tunatamani kwa hiyo maendeleo ya kazi yetu, kwa sababu yenyewe ni ya Yesu. Hayo maendeleo tunapaswa kuyatamani hata katika kazi za mashirika mengine.
Tunapaswa kupenda, kumwabudu Yesu katika masista wa shirika letu, wao ndio walio karibu zaidi na sisi, hiyo ni kweli. Lakini Bwana akituweka karibu na masista wa shirika lingine, tunapaswa sawa kumpenda na kumwabudu katika wao.
Tukumbuke tena kwamba unyenyekevu ni msingi wa wema kwa shirika letu, ambao umewekwa kwa wadogo na kwa maskini. Vazi letu ni la kimaskini na rahisi. Katiba yetu inatushughulisha kwa kutoa nafasi ya kwanza kwa masista wanaovaa shela.
Tupende kwa hiyo kujiona wadogo zaidi wa mwisho, wadhaifu kuliko Mshirika yote. Na hiyo ni nzuri kwa maskini kama sisi.
Sisi tunawaonea wivu wale ambao Mungu amewapatia kazi za maana zaidi. Tunyenyekee katika ukubwa wa udogo wetu na tufurahi kwamba Yesu anapenda kutuona angalau kazi rahisi zaidi na zisizo za maana sababu hata hizo hatustahili.
Nafasi ya mwisho kwetu sisi ni ya uhakika zaidi. Tuishike kwa upendo na katika upendo, watoto wangu wapenzi.
Msiseme kamwe, kamwe, vibaya kuhusu shirika lingine, kwanza, kama inawezekana, funikeni matendo ya udhaifu. Zungumzeni juu yao yale ambayo mnaweza kuzungumza mazuri.
Saidieni, wakati inapowezekana, kama wanahitaji. Jitoleeni, sadaka kwa ajili yao. Chochote kile mfanyacho kwa watu waliojiweka wakfu kwa Mungu, ambao ni mali yake, mnafanya kwa Yesu mwenyewe.
Pendeni haswa shirika lenu kwa sababu Yesu amelichagua kwa ajili yenu. Ni familia yenu. Katika lenyewe mnapaswa kutakatifuzwa.
Lenyewe linapaswa kuwaongoza njia ya mbinguni; kwa njia ya umaskini wake, ya kazi zake, lenyewe linapenda kuwapelekeni katika unyenyekevu mtakatifu.
Lipendeni, kama mtoto mwema ampendavyo mama yake, bali hiyo haiwazuii kupenda kwa ukweli mashirika mengine ya kitawa.
Shirika letu kwetu sisi ni mama, mashirika mengine na ukasisi ni kaka na dada zetu.
Watoto wema, wakipenda kumpendeza mama yao, wanapendana wenyewe kwa wenyewe na wanaishi kwa umoja na upendo. Na sisi, tukipenda kuwa kitulizo kwa mama yetu ambaye ni shirika, tuishi kwa umoja na kaka zetu na dada zetu, yaani ukasisi na mashirika mengine.
Tufurahie maendeleo yao, utakatifu wao, sifa zao, tusikitike pamoja nao katika masikitiko.
Tuwaendeleze, tuwasaidie inapowezekana. Hiyo itatuvutia baraka na neema tukufu, na itakuwa kwetu sisi uthibitisho ambao hatuutafuti sisi wenyewe, bali utukufu wa Mungu, kwa ajili ya manufaa ya kanisa, ukombozi wa roho.