WOSIA
XVIII. AGIZO LA KUMI NA NANE NA LA MWISHO
KUVUMILIA HADI MWISHO
"Atakayevumilia hadi mwisho" (Mt.10,22), asema Bwana.
Kitu cha maana zaidi kwa maisha ya ndani ni uvumilivu.
Wengi huanza kwa juhudi na bidii, wakitamani kwa mawazo makubwa. Lakini hawafaulu haraka, wanakufa moyo, wanaacha kazi kwa kujidai ya kwamba hawafikii kufanya chochote, kwa hiyo haina maana kuendelea.
Maskini! Uvivu na kiburi vinawashauri wao hizi sababu kwa kuacha kuendelea. Ni kujitoa kwa samahani kwa kujifurahisha ili kuacha yote.
Kumbukeni, wanangu, maisha yetu ni mashindano, kushindana hadi mwisho.
Hata kama askari labda kuanzia mwanzo alazimika kuacha hata kama akishinda kwa matokeo. Siwezi, haina maana mimi kujilazimisha.
Ina maana, mwanangu, ina maana. Haswa kwa sababu wewe unajikaza bila kutoshea kwa kuona matokeo uliyotamani, unaufurahisha Moyo mtukufu.
Jinsi utakavyoomba kwa muda mrefu, na kwa kipimo kikubwa utapewa.
Wanangu wapendwa, kwa ukosefu wa uvumilivu katika sala zetu kwa kupata neema za kiroho.
Tunahitaji neema nyingi kwa kuufikia utakatifu, lakini tunaomba kwa kutochoka?
Mara kwa mara inatokea kwamba tunaomba kutokana na msukumo wa wakati ule, mara hii moyo wa kusali, wakati mwingine upendo wa Mungu, wakati mwingine tena kwa imani kutokana na hicho kinachotujia akilini. Na kwa kuendelea hatuombi tena neema za kiroho sababu tunayo mavutio ya muda ambayo yako karibu zaidi.
Oh kama tungeweza kujenga wazo lilile wazi la kuhitaji huu au wema ule, kuweka nguvu bila maendeleo, lakini akiweza kumshinda adui kumwangusha dakika ya mwisho, ameshinda na anastahili kusifiwa na kupata zawadi.
Tusiseme kamwe kwamba haina maana kushindana. Kupigana na kuvumilia katika mashindano ni hicho kinachomfurahisha Mungu.
Isingekuwa shida kuwa watakatifu kama kila kujilazimisha kwetu kudogo kungeendelea hadi ushindi wa Mwisho.
Wakati mwingine Mungu anapenda huu uvumilivu ambao haurudi nyuma mbele ya vita na ambavyo hufanya upya kila siku na kwa amani, na utulivu, ambao husubiri hadi Mungu atampa ushindi.
Lililobaki, niaminini, unyenyekevu ungekuwa wa kukabili katika vishawishi vikubwa, kama wema ungepatatikana bila kuchoka, bila kushindana, na mara moja, Nakubali kuwa ni shida kupendana daima, na kwa hiyo kuna kuanguka daima kuinuka katika makosa yale yale. Lakini aminini pia kuwa Mungu anapendelea zaidi shindano la uvumilivu, kama ni la kuchokesha sana, kuliko ule ushindi wa rahisi na wa muda.
Watoto wangu, iweni basi wavumilivu katika maazimio yenu, wavumilivu katika majaribio ya kuwa wema, wavumilivu katika majaribio ya kuwa na huruma, wavumilivu katika sadaka ndogo.
Wakati mmoja aliulizwa Mt. Yohani Berchmans, ni kwa namna gani inawezekana kumfurahisha Maraia Mtakatifu. Yeye alijibu: "Hata kwa jaribie dogo la wema au la huruma, lakini lililofanywa kwa uvumilivu".
Mara ngapi inatokea mtu fulani, katika muda wa bidii na u moto moyoni, anafanya maazimio makubwa, na anakuwa mwaminifu kwa siku kadha, baadae moto unazimika, maazimio yanasahaulika na, baadae wiki mbili au tatu yote yanaanguka katika kusahauliwa.
Au mtu fulani anaazimia kufanya jaribio la aina moja ya kuwa mwema, kupata wema, kwa mfano katika kurudia mara kwa mara katika wazo jema. Na anajaribu kwa siku chache, na anashindwa, haoni maendeleo na anaacha yote kwa kupata, na kama tungesali haswa na labda kuvumilia katika huko kujitia nguvu, katika sala hii ya kusihi, kuomba-ikipanda mbinguni, hata kwa miaka mingi, daima jambo lile lile-kwa ukweli, baada ya hii miaka ya uvumilivu, Mungu atatukubali na atatupatia kwa kipimo kile tumwombacho.
Lakini sisi hatuna ule uvumilivu na kwa hiyo, kwamba hatupewi kile tuombacho, sababu ya ukosefu wa uvumilivu, inakuwa kuwa hatuelewi kwa kweli kile tunachohitaji. Mara moja hicho, mara nyingine kile, lakini hakuna cha maana.
Kuweni wavumilivu watoto wangu! Uvumilivu utawapelekeni kwa katika katika ushindi. Msiuache kamwe, kamwe msitake kufa moyo. Usijali, hata kama siku moja utaanguka mara mia, sababu mara mia utainuka na kuchukua njia iliyonyoka kwa utulivu na kwa imani.
Anza kila siku mwanzoni!
Sio lazima kwamba wewe uone maendeleo, sababu wewe ukiwa na nia njema. Hiyo inakutosha.
Ukiwa na nia njema, na uvumilivu utaupata ukweli Moyo Mtukufu.