WOSIA


II. AGIZO LA PILI

 

UNYENYEKEVU

 

             Watoto wangu wapenzi, angalieni unyenyekevu wa Moyo Mtukufu na muufuate.

            Sisi watumishi wa Moyo wa Yesu tunapaswa kabla ya yote, kufuata huu wema wake mpendelevu.

            Sisi watumishi wa maskini, tunapaswa kuwa wadogo sana, kwa kuvuta kwetu na kupeleka kwa Mungu.

            Rudieni kila siku, sio tu kwa mdomo lakini kwa undani wa moyo: "utufanye wadogo kama yule mdudu mdogo anayetambaa chini kwenye udongo ambae bila kufahamu miguu ya mtoto inakanyaga bila kuogopa".

            Muwe wadogo na msipende kuwa kwa sababu fulani tu, sababu maono na kujisikia kwetu kunatudanganya mara nyingi, lakini kwa maisha na kwa vitendo maana katika vitendo ndipo kwenye ukweli.

            Jaribuni kuwa wanyenyekevu na wadogo. Kumbukeni kuwa, unyenyekevu ndio mizizi ya kila wema; Wema ambao haukutokana na mzizi huu sio wema, hata kama unaonekana kwenye macho ya wanadamu. Eleweni umaskini wenu na uhafifu wenu kuwa hauonyeshi kwa maneno wala kwa kujisikia, bali kwa vitendo. Msiseme tuko wadogo lakini mnatenda vingine.

            Kabla ya yote msichukiane na yeyote, wala kwa sababu ya aina yoyote. Unyeyekevu hauchukii kwa sababu unakubali kustahili kudharauliwa na anafikiri kuwa wote wanamtendea mema mno, ambapo badala ya kuchukia anashukuru kwa kila kitu.

            Wanangu msichukiane! Kataeni kwenu kama ni kishawishi, wazo litakalowachafueni, linalowaweka pembeni, linalowakosesha heshima na jisahaumi ninyi. Hiki ni kisingizio cha udhaifu kinafanya tuachane na amani takatifu ambayo wanaifurahia wanyenyekevu. Hata wakiwafanyia mabaya semeni ninyi wenyewe kuwa, bado yote ni mazuri mno kwa sababu mngestahili motoni.

            Shukuruni kwa kila kitu, bali kamwe wanangu wapenzi mngeacha kutawaliwa kwa maelekeo.

            Kumbukeni kwamba unyenyekevu hukubali na hupokea maonyo, haujisameheshi hata kama hayo maonyo sio ya haki. Mnyenyekevu anaamini kwamba wengine wanaona zaidi yake, na anapata faida kwa yale maonyo anayopewa.

            Unyenyekevu hauzungumzi juu yake mwenyewe wala kwa mema wala kwa mabaya. Jaribuni kuzamisha kimya neno mimi. Piganeni hadi mwisho kwa tamaa ya makuu kwa sababu katika hiyo ndio mwanzo wa kuanguka kwa mtawa, katika hayo kunazalika magonjwa mabaya ya kiroho: kama chuki, wivu, ambayo yanauwa maisha ya ndani.

            Kuweni na ukuu mmoja tu: kuwa si kitu, msio wa maana, kupita katika ulimwengu kama haungekuwepo.

            Furahini kwa maendeleo ya wengine katika kazi, wakati ikiwapendeza zaidi ninyi, wakati kazi waliyopewa ni ya maana zaidi na ya juu zaidi.

            Bakini watulivu pembeni kwenu, mkikumbuka kile tu kinachowaongoza "kufuata": "Unapenda kufahamu kitu kiletacho amani kubwa? Kutofahamika na kuonekana kuwa sio kitu".

            Ni amani gani inayokaa katika moyo wa mnyenyekevu. Angalieni kutoka madhanio ambayo yanapenda daima kuwa na uhaki na kutoa kwa wengine hukumu.

            Utapoteza nini jambo likitokea kwa wengine? Kwamba yakitokea wewe hujionyeshi mwenyewe au wengine wakati wa dhambi. Nyenykeeni kwa moyo, kwa jinsi inavyowezekana, katika mapenzi ya wengine.

            Katiba yetu inasema "nyenyekeeni wenyewe kwa wenyewe"; na katika huo, kuna u nyenyekevu mmoja na kamili. Kupenda kuwa chini ya wote ni majaribu ya unyenyekevu wa kweli, ambao unamfanya mtu ajifikirie kuwa mdogo na wa chini zaidi.

            Watoto wangu, msitamani kamwe cheo au kazi nyingine na pokeeni kwa unyenyekevu, kama Bwana atawapeni, lakini msitamani kamwe. Furahini kama walio vijana zaidi wataitwa. Tiini kwa hiari wakubwa wenu hata kama ni vijana zaidi, mkionyesha kwao heshina ile mliyokuwa nayo kwa mkubwa wenu wa Novisiati.

            Watoto wangu wapendwa, kuweni wanyenyekevu, msitafute kusifiwa wala kufahamika. Kadiri mtakavyopokea kidogo kwa watu, ndivyo zaidi mtakavyozungukwa na utukufu wa mbingu.

            Pendeni, watoto wangu, kuwa wadogo, wadogo sana; nafasi iliyo na uhakika zaidi ni ya mwisho. Jifunzeni kwa Moyo wa Yesu ambao ni mpole na mnyenyekevu. Kuweni wakimya ndani na nje.

            Msifanye kelele, ongeeni kwa sauti ya chini, tembeeni na fanyeni kazi kimya kimya. Kelele ni daima, hata kama ni bila kufahamu, ni kupenda kusema kwa wote kuwa: niko mimi.

            Watoto wangu, Nawaomba: kuweni wakimya na wanyenyekevu. Mungu atakuwa pamoja nanyi na Moyo Mtukufu atabariki hakika kazi zenu na upendo mtakatifu utawaunganisha.

            Wanangu, kuweni wakimya na wanyenyekevu. Unyenyekevu ni tabia ya wema, msingi wa wa Ursula wa Moyo wa Yesu.

            Nawaomba, watoto wangu, kuweni wanyenyekevu.