WOSIA


III. AGIZO LA TATU

 

UPENDO WA KINDUGU

           

Mkombozi baada ya kuweka Ekaristia alisema kwa Mitume wake tukifuatia sisi. "Nawapeni amri mpya kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama mimi nilivyowapenda hivi nanyi mpendane ninyi kwa ninyi. Kwa hiyo wote watafahamu kwamba mu wanafunzi wangu, kama mnao upendo wenyewe kwa wenyewe" (Yoh.13,34-35).

            Watoto wangu, haya marudio ya maombi ya mzee mama yenu: Fikirini mara kwa mara, haya maneno ili muweze kuyatimiliza katika maisha na katika upendo wa kindugu.

            Kama mkiwa wanyenyekevu na wakimya kwa Moyo Mtukufu, hamtapata shida yeyote kwa kutimiza amri hii ya upendo.

            Fikirini ile furaha kubwa mfano wa upendo, ambao ni Yesu! Pendaneni wenyewe kama Yesu alivyowapenda.

            Fikirini upendo wa Yesu kwenu! Ni zipi tabia zake?  Hizi: wema usio na mwisho, sadaka hadi kifo na kifo cha msalaba.

Ambao: wema kwa mitume, kwa mikutano uliomzunguka, kwa watoto waliokuwa  wakitafuta kubembelezwa nae, kwa wenye dhambi, kwa watesaji na wauaji wake mwenyewe.

Kwa wema mwingi alizungumza nao, aliweza kuvumilia udhaifu wao, aliwasaidia, aliwategemeza, aliwaponyesha na kuwasamehe.

            Na sisi?

Kuweni wema, watoto wangu, yaani wakunjufu kwa wote.

            Kutaneni daima kwa umoja, kwa tabasamu la upendo, kwa neno moja zuri mdomoni.

            Furahini wakati mnapoweza kuwafanyia wengine kazi hata kama itawagharimu kazi kubwa au kuwakosesha raha.

            Hamwelewi ni furaha kiasi gani mnayowapa wengine kwa tabasamu la kirafiki kwa neno, moja zuri!

            Msiwahukumu wengine na kama hamwezi kukizuia kitu ndani yake, acheni kuhukumu nia ambayo ni Mungu tu anaifahamu.

            Angalieni kila mwenzenu kwa jicho jeupe la upendo na kwa hiyo mtaona yote kwa mwangaza mwema.

            Kumbukeni mambo mawili: wema unafahamu daima kushukuru kwa ukunjufu hata kwa mambo madogo zaidi. Wema unafahamu kupokea kukubali misaada midogo ya kitu chochote anachofanyiwa, hata kama hazisaidii, kwa ukarimu na kwa kushukuru.

            Waacheni wengine kwa hiari kwa kuwa na amani.

            Kuweni wema zaidi, kuweni wenye kujaa sadaka, tayari, kama Yesu kwa kutoa maisha yenu kwa wengine.

            Watoto wangu, Yesu ametoa maisha yake kwa ajili yetu: hatuwezi kujitolea na sisi, kuacha furaha zetu, kwa jinsi tupendavyo sisi, kwa kumfurahisha Yeye aliye katika wenzetu?

            Fikirini daima kabla ya yote, wengine, kama wanajisikia vizuri, nafasi zao na baadae miifikiri ninyi wenyewewe, na ingekuwa nafuu kama mkijisahau kabisa.

            Ishini kama Yesu kwa furaha ya wengine, na yawape nguvu maneno yale: "Kila wakati mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadago, mlinitendea mimi"(Mt.25,40).

            Kwa hiyo hasi, mkiishi kwa ajili ya furaha ya wenzenu, mnaishi kwa furaha na kumtuliza Yesu, Moyo wake Ulioteseka.

            Msiwe na wazo la kukata tamaa ya kuweka ahadi kila siku kwenye miguu ya msalaba: Moyo wa Yesu mteseka, napenda kukupenda nikitoa furaha kwa wenzangu.

            Ni shida labda kuonyesha furaha kati yetu? Hapana! Basi tu kuwa na moyo uliojaa upendo, tabasamu la kirafiki usoni, neno la upole mdomoni, kuwa tayari hata kwenye huduma za upendo zilizoangazwa kwa furaha takatifu. Mtakuwa malaika wa furaha, mionzi ya Jua kwa Shirika letu lote.

            Ishini watoto wangu, kwa furaha ya wengine na kwa kuutuliza Moyo wa Yesu Mteswa.

            Kama mkijaribu hivi, kimya kimya, katika upendo wa kindugu, mtapata nguvu za upendo ambazo zitawapatieni uwezo wa kutoa sadaka kubwa, kama Bwanasiku moja atawatakeni.

            Watoto wangu wapenzi pendaneni!

            Uwe mbali nanyi utengano, wivu, ambao ni adui wa kifo katika upendo, uchoyo ambao unamfanya mtu ajifikiri yeye tu akiwaona wajinga wengine, tamaa inayofanya u "mimi" kuwa sanamu, jicho baya linaloona yeye mwe-nyewe.

            Pendaneni wanangu wapendwa, hata mimi nikiangalia toka ule ulimwengu mwingine, niwaone mmeunganika kwa upendo safi zaidi kwa kuunda moyo mmoja na roho moja.

                 Hili ni agizo la moto la mzee Mama yenu ambae anawapenda toka ndani ya moyo.