WOSIA


IV. AGIZO LA NNE

 

         UMASKINI

 

            Kumbukeni watoto wangu kwamba, umaskini ni ukuta ufundishao wa roho za kitawa na kwa hiyo mnapaswa kuupenda kwa moyo wote.

            Shirika letu linapaswa kuwahudumia wadogo na maskini na kwa hiyo hata sisi, katika maisha yetu yote tunapaswa kuwa wadogo na maskini.

            Msitamani kuwa na nyumba nzuri, kubwa, zenye fahari, za kujifurahisha. Hapana,hapana! Nawasihi, watoto wangu kwamba kama wakati wa maisha yangu nyumba zetu zilikuwa maskini sana, maisha yetu mara si ya kuridhisha na chakula cha kirahisi sana, hivi hata baadae shikeni hicho kilichoandikwa kwenye sheria zetu.

            Mawazo yenu yawe daima yakielekea umaskini.

            Pendeni vazi lenu la kimaskini, na msione aibu kama kwa wakati mwingine litakuwa na kiraka basi tu liwe safi.

            Msitamani jambo la zaidi ya kawaida, furahini kama mnaweza kugawana kwa wote hicho kinachopatikana katika Jumuia. Na kama mtu fulani anahitaji kitu zaidi ya kawaida, aone ni kama kitubio na sio kukishikilia kwa moyo.

            "Safi na maskini", sio "nzuri na ya fahari, ya kujifurahisha" uwe ni msemo toka kwa maskini mtumishi wa maskini.

            Mkiwa maskini katika maisha, maskini katika kutamani, itawawieni rahisi kuuelekeza moyo kwa Mungu, hazina pekee ya moyo mkamilifu katika umaskini.

            Na kama wakati mwingine mnapaswa kuusikia kwa mfululizo umaskini kwa sababu huenda wamesahau kuwapa hicho mlichoomba, au mkifanya majaribio ya ukosefu wa kitu kibaya zaidi ya wengine, msilalamike na msiache kuchukua kwa tabia mbaya, msijiache kwa majisikio ya wivu. Furahini haswa kwa kuweza kumfuata angalau kidogo, Yesu Msalabani, Maskini aliyevuliwa hadi nguo.

            Zaidi tukiwa maskini, ndipo zaidi twaweza kuelewa maneno ya mt.Fransis, maskini wa Assisi: "Mungu wangu na yote yangu".

            Kadiri tutakavyohitaji vichache kwa ajili yetu wenyewe, ndivyo zaidi tutaweza kutoa kwa maskini.

            Kwa umaskini na kwa kushikilia sana kazi Tuko maskini na kwa tunao wajibu wa kupata mkate kwa ajili yetu wenyewe na kwa ajili ya watoto wetu maskini.

            Kazi, kazi ngumu ya maskini ndio wajibu wetu.

            Kama maskini anavyofanya kazi kwa jasho lake usoni, hata kama mifupa yamuuma na anasumbuliwa na usingizi sababu anajua anapaswa kufanya kazi, kwa vingine yeye na watoto wake watabaki bila mkate, hivi hivi hata sisi tunaopaswa kufanya kazi.

            Hatukuja hapa ili tuchoke kidogo zaidi ya walimwengu, bali tumekuja ili tufanye kazi zaidi na ngumu zaidi.

            Katika ulimwengu tulifanya kazi kwa ajili yetu, badala yake huku tunafanya zaidi kwa makusudi ya Mungu ambae amechoka sana kwa ajili yetu na ametoa kwa ajili yetu maisha yake.

            Tusione aibu ya kufanya kazi. Hakuna kazi inayomshusha mwanadamu.

            Nenda kwenye ile kazi uliyopewa kwa utii bila kujiuliza ni ya maana zaidi au hapana, ya kunyenyekesha, au ya juu na ya heshima.

            Fanya kazi kwa ajili ya Mungu pekee, na uwe daima, daima tayari kwa kazi yoyote ile.

            Mungu awaepusheni kuwa kati yenu yeyote aonae hastahili sababu amepewa kama asemavyo yeye, kazi, ya unyonge zaidi.

            Kadiri zaidi kazi ilivyo ya unyonge ya kunyenyekea mbele ya macho ya wanadamu kadiri ilivyo ya kujificha, kadiri ilivyo ya uchovu na kuchokesha kadiri ilivyo na heshima kidogo, ndivyo zaidi itakuwa ya maana, kama mnayo roho ya kimaskini.

            Fanyeni kazi kwa bidii kwa ajili ya Mungu!

            Kazi zenu zinasaidia kwa kuwatunza mayatima wetu. Tukumbuke kile alichosema Bwana: "Kila wakati mlivyomtendea mmo jawapo wa hao ndugu zangu wadogo zaidi mmenitendea mimi" (Mt.25,40).

            Wazo ambalo kwa kufanya kazi ni kwa kuwatunza mayatima wetu, tunafanya kwa Yesu mwenyewe, haituamshi zaidi na kutupa nguvu daima kuwa wenye bidii zaidi na kujitoa bila mwisho kwa kazi yetu?

            Katika umaskini na katika kazi, hata kama ni ngumu na ya kuchosha, napendelea kuwaoneni, watoto wangu wapendwa.

            Nawaomba na nawasihi wale niwafahamuo na ambao mimi mwenyewe nimewaongoza, na wale nisiowafahamu sababu mtaingia katika Shirika baada ya kifo changu-lakini niwapendao kama ningeliwafahamu: pendeni umaskini, utamanini umaskini.

            Mimi kwa juu nitasali ili kamwe katika nyumba zenu kusiingiwe na utajiri, unadhifu upelelezi, starehe. Hapana, hapana! Tuko maskini na tubaki maskini.

            Kumbukeni kwamba ni afadhali kuhitaji kidogo kuliko kuhitaji zaidi. "Mungu wangu na yote yangu"-Haya utajiri wetu.