WOSIA


V. AGIZO LA TANO

 

  UTII

 

            Kama unyenyekevu ni mzizi wa kila wema, hivi utii ni msingi wa kila wema wa kitawa.

            Kama mnapenda kuwa wema na watawa watakatifu, jaribuni kuotesha ndani yenu utii kamili. Utii unapaswa kulishwa na imani, bila hivyo hautakuwa kamwe kamili.

            Mnapaswa kuamini kabisa kwamba Mungu katika utu wa mkubwa wenu anaongoza nyumba zenu, kwamba Mungu kwa njia wa wakubwa wenu, anawapeleka, anawaongoza njia ya kufuata, anawafunulia mapenzi yake.

            Uamuzi wa viongozi ni Mapenzi ya Mungu kwa Masista.

            Kwa hiyo, heshimuni pendemi, tiini, msifunni Mungu katika wakubwa wenu.

            Katika nyumba zetu zote, iwe kuu au uwanda wa kati au jumuiani ndogo, utu wa mkubwa au kiongozi uwe umezungukwa na heshima kubwa na upendo, na hiyo ni kwa ajili ya Mungu.

            Wanangu, mmemzunguka kwa heshima kubwa Mama yenu mzee, na mimi daima nilielewa kwamba, chochote kile chema mlichonifanyia, kwa Mungu mmefanya, na kwa Mungu hakuna chochote kilichozidi.

            Hicho mlichekifanya kwa Mungu katika utu wa mzee Mama yenu, wapeni kila mkubwa au kiongozi sababu katika wao mnamisfu Mungu, ambao ni sawa sawa heshina iwe ni kwa mzee Mama yenu, iwe ni kwa mkubwa aliye kijana au kiongozi.

            Shirika letu, ambalo msingi wa wema wake ni unyenyekevu, unapaswa kututofautisha kwa heshima, staha wanazopewa wakubwa.

            Msifikiri kwamba, umri unatuzuia kutumia heshima, kwa mfano: kupiga magoti mbele ya mkubwa kupiga magoti haipo tena kwenye Sheria, wakati unapoomba kitu fulani, wakati yeye anatuonya, wakati wa kuomba msamaha au baraka, au kuinuka wakati mkubwa anaingia darasani, mezani au kwenye vyumba vingine nk: au kuomba msamaha na kushukuru mezani, nk.

            Hata katika umri mkubwa wa sista, hata umri wa kijana lakini mkubwa au kiongozi inatolewa hiyo. Mungu yule yuko kwa wazee na pia kwa vijana wakubwa zetu.

            Na sisi wazee na vijana tuko daima "wadudu wadogo" mbele za Bwana ambapo kwanza tunapaswa kusujudia kwa unyenyekewu wa moyoni.

            Kwanza, walio wazee zaidi waonyesha mfano mzuri kwa walio vijana, wakiwafundisha wao kwa matendo ni kwa namna gani wanapaswa kuzunguka kwa heshima wakubwa wao, sababu katika wao twamsifu Mungu.

            Vijana, wakubwa na viongozi waelewe kuwa hizi alama za heshima katika sheria za Shirika letu, zinatolewa kwa Mungu, katika utu wao, na waelewe kuwa hawana haki, kwa unyenyekevu wa uongo kusamehe masista bila maana, sababu zile alama za heshima na upendo hazitolewi kwao, bali kwa aliye Juu.

            Kama mnapenda mapenzi ya Mungu mtapenda utii ambao unawapa uwezo wa kutimiza kila wakati mapenzi ya Mungu.

            Msipende kujiunga kuwa na namba ya zile roho zinazopenda utii wakati tu mapenzi ya wakubwa yanapatana na yao wenyewe, lakini hata wanachukia na kunung'unika wakati mapenzi ya wakubwa sio wapendavyo wao. Hapana, hapana!

            Tiini daima, japokuwa mapenzi ya wenye madaraka yanawapendeza au hapana; katika wao mtakutana na mapenzi ya Mungu, na hivyo inawatosha.

            Kuweni tayari kwa kila maelezo ya mapenzi ya wakubwa wenu na katika kila amri jibuni daima: "Mimi hapa mtumishi wa Bwana" (Lk.1,38). Kama Mungu apendavyo!

            Pendeni ule utii mtakatifu!

Usifuni, uheshimuni na tiini wakubwa wenu na Mungu atakuwa pamoja nanyi, wanangu wapendwa.

            Nawaombeni kwa unyenyekevu, timizeni agizo hili la mzee Mama yenu, sababu hata katika lenyewe ni kwa kweli kwenu ni mapenzi ya Bwana.

            Tiini kwenye mambo madogo, tiini kwenye mambo makubwa, tiini daima na popote. Mnapokuwa wazee zaidi, hivyo zaidi zidini kutii.

            Tena kitu kimoja nawaomba, watoto wangu wapendwa, sikilizeni kwa heshima, kwa unyofu na upendo, mikutano ya wakubwa. Hakuna atakayefikiri kwamba hahitaji, kufahamu zaidi jinsi ya kujichukulia. Msitoe sheria ya kutayarisha kila jioni juu ya kutafakari kwamba fikara za mkubwa hazikubaliani nanyi.

            Hapana, watoto wangu, hapana! Katika hiyo kuna uharibifu mkubwa wa kiburi, kumbukeni kwamba Mungu anawazungumizeni kupitia kwa wakubwa.

            Sikiliza kwa unyenyekevu, kubali kuwa unahitaji mashauri ya mkubwa. Na hata kama mara kumi huoni chochote kinachopatana na wewe mwenyewe, inawezakana mara ya kumi na moja Bwana atatumia maneno yake yeye mkubwa kwa kuufumbulia moyo wakohazina za Moyo Mtukufu, zile hazima ambazo, mwenyewe labda, kamwe usingezigundua.

            Kama utii wenu unatokana na imani; haitawawia vigumu kuyatimiza mapenzi ya Mungu yaliyoelezwa kwenye mapenzi ya wakubwa.