WOSIA


VI. AGIZO LA SITA

 

SALA

 

            Hatupaswi kuishi kwa ajili ya dunia bali kwa ajili ya mbingu. Na kwa mbingu ni kuishi kwa kujiunga na Mungu kwa sala.

            Sala kwa kweli ni daraja linalounganisha kati yetu na u milele, dunia na mbingu, mwanadamu na Mungu. Na kwa hiyo maisha ya mtawa yanapaswa kuwa maisha ya sala.

            Nafasi ya kwanza ni kufuata kwa u hakika u sawa mazoezi ya kiroho inavyoelezwa kwenye Katiba yetu. I napowezekana, msiache bila sababu maalum. Huu ndio kweli, wajibu wenu kwa aliye Juu.

            Mungu awaepushe msiziache, kwanza mzifuate kwa utafiti kabisa wa juu.

Apendae kwa kweli, anafanya, anajaribu, na anapata kwa kawaida; muda kwa huu muda wa maana ambao ni wa mazoezi ya kiroho.

            Utakuwa ndio utatuvutia neema, mwanga, msaada wa Mungu, utakuwa ndio uta washushia kwa maisha yenu yote baraka zake. Bila sala hakuna maisha kwa ajili. ya Mungu hakuna huduma kwa mungu!

            Watoto wangu, fuateni kwa imani kweli kweli mazoezi ya kiroho hila kuangalia kwamba mnapata kitulizo au mwako. Sio kwa kujitosheleza kwenu, bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu muwe waaminifu katika hiyo, mkipigana kwa ushujaa dhidi ya kusahau ulegevu, uvivu unaofanyika kwa kujifanya kwa njia mbali mbali, ili kujitoa katika sala.

            Salini kwa imani na kwa juhudi siku kwa siku!

Sista ambae ni mwaminifu katika ukimya, asiyefanya uchunguzi wala kujiingiza katika mambo ya wengine, anapata muda wa kutimiza wajibu wake wa kiroho.

            Inawezekana kutokea wakati mwingine hata hiyo. Kwa hiyo, wanangu, ambeni daima ruhusa. Na kama hamna muda wa kuomba mwapaswa kwa mara ya pili, mpatapo wasaa mumweleze mkubwa wenu.

Msizoee kujiruhusu wenyewe.

            Kristo alisema kwamba tunapaswa kusali daima, bila kuchoka (cfr.Lc.18,1).

Msijiwekee mpaka kwa mazoezi ya kiroho tuliyoombwa kwenye Katiba yetu. Hapana, hiyo ni kidogo mno kwa roho! Tafuteni kwa mfulilizo umoja na Mungu kwa kuwa na nia nzuri, inayofanywa upya mara kwa mara, kwa mfulilizo wa sala fupi, zikiongoza mawazo yenu, hata wakati mkiwa kazini, kwa Mungu Yesu wenu, kama ua linalo elekea jua.

            Haya furaha ya roho: kuwa katika Mungu na pamoja na Mungu.

            Kwa hiyo cho chote kile cha duniani kionekanacho kidogo sana, chepesi, mahangaiko, umaskini na mateso ya maisha haya panawaka daima mionzi ya amani, ya matumaini, ya furaha.

            Katika hii sala ya mfulilizo inahitaji majaribio bila Kufa moyo, kama haitokani kwamba mnaipendelea, Inahitaji kujaribu, na kujaribu na kujilazimisha na hiyo ni kazi- kama imefanywa kwa upendo- itakubaliwa na Mungu, hata kama inaonekana haina matunda.

            Salini daima kwa imani. Haya lililo shauri langu, watoto wapendwa; msiwe na muda wa kupoteza, mwanzoni mwa kila sala wekeni nia thabiti na imani ya kweli ya ndani.

            Kadiri zaidi itakavyoingia akilini mwenu kwamba Mungu nakuona, kwamba tuko nae, kwamba tunasali chini ya miguu yake, kwamba tunajishikilia kwenye Moyo mtukufu, ndivyo zaidi sala itakuwa rahisi na itachukuliwa.

            Salini kwa imani bila mwisho na kwa uvumilivu. Mungu atatupa kwa kweli hicho tumwombacho, kama kinaleta manufaa mema ya kiroho, lakini inapaswa kusali bila kuchoka, hata kwa miaka mingi, kwa hakika ya moyoni, kwamba Baba mwema wa mbinguni atatupatia hicho tunachomwomba kwa jina la Bwana Wetu Yesu Kristo.

            Kama tungekuwa na imani kubwa, tungeweza kuihamisha milima. Salini kwa upendo uwakao, kama sio kwa kujisikia, bali kwa hiari. Tafuteni kumpenda Mungu Mwenyezi, Baba yetu mwema, jaribuni kumpenda Mwokozi wetu msulubiwa, tafuteni kumpenda Roho Mtakatifu ambae awatakatifuzeni, tafuteni kuupenda Utatu Mtakatifu, jaribuni kumpenda Maria, Mama yetu.

            Kadiri mlivyo na juhudi kidogo na wepesi wa kuona, hivyo zaidi tamanini, hata hwenye moto, kuonyesha kwa Mungu kwa ustahimilivu ule upendo ambao hamkuweza kuusikia.

            Salini kwa mfulilizo, watoto wangu, kama anavyopenda Yesu. Toleeni kwa Mungu matendo yenu kupitia kwa sala fupi za mara kwa mara; mkiinua mara kwa mara macho ya mioyo kuelekea tabernakolo, kuelekea msalaba.

            Nawashaurini kwa namna ya pekee haswa kitu kimoja: Pateni faida kwa uangalifu, japokuwa kuna uvivu wa asili, muda unaopotezwa- "les moments perdus". Wakati mnaposubiri, mtembeapo njiani, toka sehemu moja kwenda nyingine, salini, salini.

Hizi ni nyakati ambazo hakuna kufikiri chochote cha maana, ambapo mawazo yanakuzunguka pembeni yako mwenye we kama kwenye caleidoscopio, au labda uko kwenye matatizo au kwenye maazimio ya baadae. Mtafanya mengi zaidi mkisali.

            Oremus, tuombe watoto wangu!

Siwezi kuwashaurini chochote kilicho nafuu zaidi.

            Maisha yenu yatabadilishwa kwa sala na Mungu atakuwa pamoja nanyi.

            Katika sala mtampata yeye mnayempenda Katika sala mshikilieni kwa nguvu na msimwachilie (cfr. Ct.3,4).