WOSIA
VII. AGIZO LA SABA
UPENDO KWA MSALABA
Watoto wangu wapenzi, kwa mtawa, upendo kwa Yesu msulubiwa ungepaswa kuwa roho ya maisha yale ya ndani, roho ya moyo wale.
Kumbukeni kwamba toka kwa ule mti mtakatifu wa msalaba ndipo ilipotoka sadaka ile kuu ya upendo kwa moyo wa binadamu. Yesu msulubiwa kwa mateso, na kifo chake, ametustahilia neema na neema: Eukarestia Takatifu. Kwa kweli Missa takatifu ni tendo la kutimiza tena sadaka ya Yesu juu ya msalaba.
Juu ya msalaba Yesu wamemtoboa moyo kwa kuufanya uwe makimbilio, ulinzi na mbingu ya roho, sababu toka moyo huu ndio kisima chetu ambacho na mfulilizo wa kutoa upendo.
Juu msalabani Yesu ametupa Maria kama Mama na ametutoa kwa Maria kama watoto.
Juu msalabani zilishuka neema kwa utakatifu ambao ziliwatakatifuza, ambao kwa maombezi yao makubwa wametupatia namna ya kuwa wema na watakatifu.
Chochote kile kilicho kizuri kitukufu na kitakatifu katika maisha yapitayo ya kawaida kimeshuka kwenye msalaba sababu Kristo ametustahilia yote hayo kwa mateso yake na kifo chake.
Na kwa hiyo watu waliojiweka wakfu wanapaswa kuinua macho yao kuelekea msalaba, kama ua lielekeavyo jua.
Katika msalaba upo wokovu wetu, katika msalaba yapo matumaini yetu katika msalaba upa upendo na furaha, katika wenyewe kila jema letu.
Sababu juu msalabani Yesu ametukomboa kwa Damu yake Takatifu, ametufungulia milango ya mbinguni; kwa mateso yake ametuhakikishia furaha ya milele.
Ni upendo gani, ni shukrani gani twapaswa kutoa kwa Mkombozi wetu!
Ulimwengu unafikiri kidogo kuhusu shukrani hizi, unawaza kidogo kuhusu huo upendo, sababu wenyewe unadai upendo kwa upendo sadaka kwa sadaka; Sababu msalaba unaonekana kutufanya tutafiti na kupaswa kuutuliza Moyo mteswa wa Kristo, kupaswa kuchukua pamoja nae msalaba, sababu masikitiko yake na machozi yake hayawezi kutufanya tukiri kwa furaha hii ya juu juu ya ulimwengu.
Kwa nadhiri takatifu tumepigiliwa kwenye msalaba na tunalo Sharti la la kumfuasa Yesu Msulubiwa- maskini na Yesu maskini, wachovu na Yesu mchovu, msalabani pamoja na Yesu Msalabani.
Kwa mtawa, msalaba ni furaha yake yote, ni upendo wake wote, ni chochote kile chake. Ameuacha ulimwengu na vyote ambavyo ungeweza kumpatia. Badala yake amepokea msalaba na katika huu anapata kile ambacho anaweza kutamani: kwa hiyo Shikilieni sana msalaba tu, tafuteni furaha, faraja na kitulizo katika uchungu, mwanga kwenye giza ushauri kwenye mashaka, kitubio kwenye kuanguka, utulivu kwenye dhoruba ya maisha, matumaini kwenye mkato wa tamaa furaha wakati wa kifo.
Watoto wangu, mpendeni Yesu msulubiwa, mpendeni kwa moyo wenu wote. Jishikeni kwenye miguu yake, bakini na Yeye kwa mawazo na kwa moyo.
Tafakarini mara kwa mara Mateso ya Bwana. Jifunzeni kwa Yesu msulubiwa jinsi ya kumpenda Mungu, jinsi ya kuwapenda wanadamu, jinsi ya kuwa wanyenuekevu, watii na wanye kujitolea, jinsi ya kujitoa sadaka kwa wengine, jinsi ya kufanya kazi kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kwa ukombozi wa dunia.
Njia bora zaidi ya kumtuliza. Yesu msalabani ni kumwonyesha upendo wako haswa, na kuiga wema wake.
Kadiri mtakavyo jaribu kumuiga Yesu msulubiwa, kadri mtakavyo kuwa karibu zaidi na msalaba, ndivyo zaidi Msalaba utakuwa ni kila kitu kwenu duniani. Hata wakati wa Missa, tafakarini mateso ya Kristo.
Fanyeni kwa hiari Njia ya msalaba, busuni mara kwa mara msalaba kwa upendo mkubwa na jifunzeni kwamba katika msalaba kuna raha kubwa raha ya mbingu kati ya uchungu wa ulimwenguni.
Kwenye kanisa kuu la Mt. Maria wa Malaika Roma nimeyakuta maneno yafuatayo ambayo yamekuwa katika maisha yangu kitulizo kikubwa, mwanga na utulivu na nayatoa kwenu: Kwenye miguu ya Yesu kuna waridi wa miiba ni vizuri kuteseka ni furaha kufa.