WOSIA


VIII. AGIZO LA NANE

 

IBADA KWA BIKIRA MARIA

 

            Katika huo wosia wangu kuacha baadhi ya kurasa nyingine kwa Mama yetu, Malkia na bibi, Maria Mtakatifu.

            Mpendeni Maria, mpendeni kwa upendo, mpendeni kweli. Kweli kama watoto wazuri, mpendeni huyu Mama yetu. Yeye tumepewa toka kwa Mungu.

            Yesu juu ya msalaba ametuachia kama, urithi Maria. Mapenzi ya mwisho ya Yesu ni kwamba sisi tuwe watoto wema wa Maria.

            Kwa hiyo tuelewe hivyo, tusali na tujaribu Kwa nguvu zetu zote kuwa hivyo.

            Maria kweli ni Mama mwema na mwnye huruma yeye anatamani zaidi yetu, kuhusu ukombozi wetu.

            Kwa hiyo mkimbilieni yeye kwa imaniya kitoto. Msiruhusu kamwe kwambakunajificha mioyoni mwenu kutokuwa na uhodari, ukosefu wa matumaini, kuweni na uhakika kwamba Maria, kwa kuwaletea msaada, atafanya muujiza kuliko kuwaacheni.

            Kama mtoto kwenye mikono ya mama yake, hivyo hata ninyi, bakini kwenye miguu ya Maria kwa amani, hata japokuwa wakati mwingine dhoruba inafurika.

            Pendeni kile kimpendezacho Maria. Pendeni rosari. Msiiseme tu kwa maneno, bali kwa maisha yenu yote, mkijiigiza kwenye wema wa Maria yaliyosemwa kwenye mafumbo ya Rosari. Kusali rozari kiwe ni kitendo cha juhudi na upendo kwa Maria, iwe ni kutupa juhudi kwa wema wake, uwe ni utafiti mmojawapo juu ya imani katika kuufuata mfano wa Maria, ni sala kwa kupata utakatifu kutokana na utakatifu wa Maria.

            Kuweni daima na rozari pamoja nanyi, mchana na usiku, msiiache kamwe. Iwe ni rafiki yenu mwaminifu, mnyororo wa kuunganisha moyo wenu na moyo wa Mama yetu mbinguni.

            Na yawe haswa ya thamani maneno ya Maria yaundayo neno la Shirika letu: "Tazama mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu hicho ulichosema" (Lc.1,38).

 

            Jaribio kubwa kwetu kwa Maria ni kuufuata wema wake. Pendeni basi kama yeye, ambae ni mtakatifu na safi, kuwa waaminifu na watumishi wa Bwana, daima tayari kwa kuyatimiza mapenzi yake, awe yeye mletaji wa furaha popote kwenye misalaba na uchungu.

            Mapenzi ya Mungu! Kama Maria alivyokuwa akisalimu kila tamko la Mungu kwa maneno: "Tazama mimi ni mtumishi wa Bwana...", yaliyosemwa nae siku moja na kuyarudia kwa maisha yake yote kwa moyo na kwa vitendo, hivi hata ninyi watoto wangu, kuweni kama yeye daima, katika mzunguko wa maisha, watumishi wanyenyekevu wa Bwana wanaoyapokea daima mapenzi ya Mungu, popote pale walipo, kwa tabasamu mdomoni, kwa "Fiat" na "Deo gratias" moyoni, hata kama na machozi machoni - kama Maria.

            Na kama mapenzi ya Mungu yakiwaelemea kwa uchungu mkali, kama mtakosa nguvu kumshukuru kimya kimya, basi inueni macho ya mioyo yenu kwa Maria kwa Mama yenu mwenye huruma na ombeni:

Ee, Mama tufundishe kuwa wakimya daima watumishi wa Bwana, wanootamani kitu kimoja tu: Mapenzi ya Mungu yatimie na sio yangu yatimizwe.

            Mpendeni Maria, watoto wangu, pendeni rosari na niaminini: Upendo bora zaidi kwake ni ule wa kuwa yeye mkimya, mwaminifu, mtumishi mnyenyekevu wa Bwana anayerudia mfululizo kwa moyo na kwa matendo:

Tazama, na yatimizwe kama Mungu apendavyo,

kama Mungu apendavyo!