WOSIA


IX. AGIZO LA TISA

 

    KUJIHINISHA

 

            Watoto wangu, tafakarini mara kwa mara Moyo Mtukufu wa Yesu uliochomwa kwa mkuki, uliovalishwa taji ya miiba. Sikilizeni yale malalamiko ya uchungu wa Kristo mteswa: "Nimetafuta wa kunituliza lakini sikupata".

            Tafakarini ule moyo ulionyweshwa uchungu, fedheha, mateso, na eleweni kwamba anayeupenda ule Moyo anafahamu kujinyima na haswa haachani kabisa kuunganika: na upendo wa msalaba.

            Msifikiri kuwa mnatakiwa kujinyima sana na kufanya vitubio vikubwa zaidi ya kawaida. Hapana, hapana watoto wangu! Mimi, katika wito wetu niko mbali kabisa na mtindo wowote wa kigeni, usio wakawaida unaotutoa katika kazi zetu na katika umaskini wetu.

            Nawapa uhodari kwa yale tunayokutana nayo kila siku hatua kwa hatua, ambayo ni ya lazina kwa kutenda mema kwa matendo yetu, yale tunayohitaji kwa kuishi kwa amani katika upendo na katika utii wa kitawa. Huo ningesema, ni kujinyima kwa ukarimu ambao hauonekani kwa macho, hauvutii uelekevu wa watu kwa hiyo ni wa hakika zaidi, kwa hiyo hauleti vishawishi vya upuuzi vya kujisikia uko juu ya wengine.

            Maisha ya kitawa yanapaswa kuwa maisha ya kujinyima. Maisha bila ya kujihinisha sio maisha ya kitawa.

            Kujihinisha kwa kwanza, watoto wangu, ni kuwa waaminifu katika kuitekeleza katiba yetu. Yenyewe ni kilele kwetu sisi ambacho twapaswa kukifikia na kwa hiyo ni kujihinisha.

            Kwa wangalifu huo huo wa kutoacha maelezo ya kwenye katiba ni pia kujihinisha kwa uhodari.

            Waalimu wa maisha ya kindani ya roho, wanahakikisha kwamba maisha ya mtawa anaetimiza kwa uaminifu Sheria takatifu ni maisha ya kishahidi. Kabla ya yote fanyeni kujihini huku.

            Fanyeni kwa hiari huku kujinyima kutokana na vitendo vya kila wema. Hakuna wema bila ya kujinyima.

            Mtu mmoja mfikiri sana wa ki-katoliki, Madame Swétchine, alisema kwamba wema ambao haukugharamiwa hauna maana yeyote.

            Kwa kujinyima ni kifo cha pole pole kwa asili yetu ya ubinadamu, ni kuishi kinyume cha nia yako, uthamani wako, mapenzi yako, kwa kulikanyaga neno "napenda" na "sipendi", kwa kutimiza zaidi kile kinachompendeza Mungu.

            Msicheze cheze na mahinisho, kujinyima mambo madogo ya kitoto, na kuacha kufanya yale ya kweli yanayoleta mema.

            Lakini kujinyima kwa mambo madogo lakini iliyofanywa kwa upendo wa Mungu, inaleta faida kwa roho ikiwa haiondoi yale ya maana ambayo ndio yanaleta wema wa kweli.

            Wakati wageukapo na kubuni mahinio madogo madogo baadae wanaachilia kuyafanya yale yaliyoelezwa, kazi, maisha ya Jumuia. Hata hayo ya kwanza kama ni mazuri, haya ya mwisho ni ya maana zaidi na ya uhakika zaidi sababu hayatupeleki kwenye upuuzi.

            Fanyeni mazoezi kwa uhodari katika kujinyima kwa yale ya maana zaidi, ambayo ni sehemu kamili ya mazoezi ya kila wema.

            Unahitaji kujihinisha kwa kuishi vyema na kwa mkazo wa fikira, kwa kufanya kazi kwa juhudi, kwa kutii na kuwa tayari, na mwenye ushujaa, kwa kuweza kuushika moja kwa moja utulivu wa moyo.

            Hizi nafasi huhitaji kuzitafuta; zinajileta zenyewe ili uweze kuzitumia.

            Kujihinisha kwingine ni: kuweza kuchukua kimya kimya na kwa hiari misalaba midogo ambao Mungu anakutumia: ni upendo wa msalaba.

            Maisha yanaye msalaba wake, kila wakati msalaba mkubwa zaidi, bali siku kuna misalaba midogo, kama sindano, ambayo yote hayo ni maumivu na uchungu moyoni.

 

            Yapokeeni kwa mikono wazi, watoto wangu, hii misalaba midogo. Ni Mungu anawatumieni. Ipendeni kwa moyo wenu wote sababu inatuongoza kwa Mungu kwa uhakika zaidi ya kufarijiwa kukubwa.

            Na mbele ya misalaba mikubwa inayoiaza maisha yetu uchungu na mateso, pigeni magoti kama Mtakatifu Andrea mkisena: "Salamu msalaba mtakatifu, matumaini yangu ya pekee, Salamu!".

            Jaribio zuri zaidi la upendo ambalo tunaweza kutolea kwa Mungu, ni kuweza kuchukua kwa hiari misalaba yetu. Hakuna upendo mkubwa zaidi ya huo.

            Itakuwaje usiupende msalaba unaotusaidia kusema kwa Mungu: Bwana wewe unaona kwamba nakupenda!

            Pendeni kila msalaba, mdogo au mkubwa uwao wowote, na hata ule msalaba mdogo ambao labda utakuwa kwenu, yaani kifo cha mzee Mama yenu.

            Pendeni misalaba yenu midogo, kila mmoja wa hii ni masalio matakatifu ya msalaba wa Kristo na kwa hiyo twapaswa kuu-shikilia kwa upendo na kuuchukua kwa furaha takatifu.

            Misalaba ambayo Mungu anatupa, midogo au mikubwa, ni shule nzuri zaidi ya kujirudi.

            Chukueni misalaba kwa hiari, kimya kimya, kwa utulivu, huku ndiko kujitoa kunakopokelewa zaidi na Mungu; hatuwezi Kufikiri chochote kingine cha maana zaidi.

 

            Kwa hiyo, iweni na juhudi wanangu wapendwa: semeni daima kwa furaha: "Salamu msalaba mtakatifu, tumaini langu la pekee".