WOSIA
MANENO YANGU YA MWISHO KWA WATOTO WANGU WAPENZI
Kazi hiyo, maagizo hayo ambayo nimewapeni, yamekwisha, watoto wangu wapendwa.
Ningependa kuwaombeni bila kukoma wanangu: tafuteni kwa nafasi ya kwanza utakatifu. Hilo ndilo kusudi ambali mmelijia mlipoingia Shirikani, haya ndio mapenzi ya Mungu: kujitakatifuza kwenu.
Iweni watakatifu, na baraka ya Mungu itabaki katika shirika lenu. Iweni watakatifu na kwa urahishi mtawavuta wengine kwa Mungu. Iweni watakatifu na furaha tukufu itakuwa Iweni. Iweni watakatifu na mtakuwa watulizaji wa Moyo wa Yesu katika mateso. Iweni watakatifu!
Ni kwa furaha gani nitaangalia toka mbinguni watoto wangu ambao hujitahidi kwa bidii katika njia ya usahihi.
Tafuteni kabla ya yote ufalme wa Mungu na haki yake (Mt.6,33).
Na tena kwa mara nyingine nawaomba, watoto wangu, ishini kwa umoja, kwa kupatana, kwa upendo wa moyo, uliolindwa kama Wakristu wa kwanza, "Moyo mmoja na roho moja" (At. 4,32).
Pale panapokosekana umoja na usikizano, hamwezi kupata baraka ya Mungu wala utakatifu.
Iweni wanynyekevu, na fahamuni kuutunza huo upendo mtakatifu, huu usikizano na umoja katika Mungu.
Ni afadhali kwa adhabu ya kimwili, kwa matokeo ya kutokuwa na wema kama wengine, ili upendo wa kindugu usijeharibika.
Mnapenda kazi iongezeke?
Ishini katika upendo na usikizano. Mnapenda kuwa watakatifu?
Ishini katika upendo na usikizano. Mnapenda kuwawuta wengine kwa Mungu? Ishini katika upendo na usikizano.
Hakuna chochote kinachoweza kusemwa kwa moyo wa kibinadamu kwa ajili ya Shirika la watawa lililounganika kwa kifungo cha usikilizano na upendo wa kindugu.
Jaribuni hivyo kwamba, masista wajisikie vyema pamoja nanyi. Saidieni mawazo yao kwa yale yawatiayo huruma kwa wajibu wenu. Wekeni mbele furaha yao kwa yenu na Mungu kwa baraka yake atakuwa pamoja nanyi.
Naamini kwamba nitalia mbinguni, kama nitawaona wanangu waliotengana, ya kwamba wanashindana na hawapatani kati yao. Ni afadhali kwamba Shirika letu liache kuendelea kuliko iitokee utengano na kutosikilizana Mungu awaepusheni.
Na sasa nawaaga tena kwa mara nyingine watoto wangu.
Nawaomba kama mnanipenda, onyesheni upendo, heshima na utii kwa yeye atakayenipokea, kama kifo kitanikuta katika cheo cha Ukuu wa Shirika, Mama Generali.
Msiyafanye magumu, maisha ya mkubwa wenu. Rahisisheni daima, daima nawaomba kwa moyo wote. Mungu awe nanyi! Salini kwa roho yangu masikini yenye dhambi.
Msimsahau Mzee Mama yenu ambae atawapenda daima na daima atasali kwa ajili yenu, na daima atabariki watoto wake: kwa Jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu. Amina.
Pniewy, Sant'Olaf, 28.10.1924